Zephaniah 2:8-10

Dhidi Ya Moabu Na Amoni

8 a“Nimeyasikia matukano ya Moabu
nazo dhihaka za Waamoni,
ambao waliwatukana watu wangu
na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao.
9 bHakika, kama niishivyo,”
asema Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mungu wa Israeli,
“hakika Moabu itakuwa kama Sodoma,
Waamoni kama Gomora:
mahali pa magugu na mashimo ya chumvi,
nchi ya ukiwa milele.
Mabaki ya watu wangu watawateka nyara;
mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”

10 cHiki ndicho watarudishiwa kwa ajili ya kiburi chao,
kwa kutukana na kudhihaki
watu wa Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Copyright information for SwhNEN